Radio Jamii Kilosa

Kuelekea Siku ya Wanawake duniani wanawake wametakiwa kuchangamkia mikopo nafuu Kilosa

1 March 2023, 9:20 am

Afsa Maendeleo ya Jamii Bi Neema Solomon akiwa ofisini kwake. Picha na Asha Mado

Machi nane mwaka huu wanawake wameshauriwa kujitokeza kwa wingi ili kujiunga katika vikundi ambavyo itawawezesha kupata mikopo kwa urahisi kupitia asilimia 4 ya mikopo inayotolewa kwa wanawakekutoka serikalini ambayo itawawezesha kubuni ama kuendeleza miradi ambayo wanayo na kuwasaidia kuwakwamua kichumi na kujiletea maendeleo wenyewe.

kama idara ya maendeleo ya jamii tumeamua kuitumia siku hii ya wanawake duniani kuwakutanisha wanawake, vijana na makundi maalumu yaani watu wenye ulemavu ili kuwapatia elimu ya mikopo kutoka katika taasisi za kifedha“.

Na Asha Mado

Kuelekea siku ya wanawake duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Machi 8 ya kila mwaka wilayani Kilosa maadhimisho hayo yatafanyika katika kata ya Parakuyo ambayo yataambatana na utoaji wa elimu ya masuala ukatili pamoja na kumkomboa mwanamke kiuchumi kupitia vikundi ambavyo itawawezesha kupata mikopo.

Akizungumza na Redio Jamii Kilosa ofisini kwake Afsa Maendeleo ya Jamii kitengo cha wanawake Neema Solomon katika maadhimisho hayo kwa mwaka 2023 yaliyobeba kaulimbiu isemayo Ubunifu na mabadiliko ya teknolojia chachu katika kuleta usawa wa kijinsia yatawakutanisha wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ili kuwawezesha kutambua fursa za mikopo.

“Wanawake wengi bado wanachangamoto nyingi wanazokutana nazo hususan kushindwa kujikwamua kiuchumi kutokana na kukosa fursa za kuwawezesha mitaji na elimu ya mikopo hivyo kama idara ya maendeleo ya jamii tumeamua kuitumia siku hii ya wanawake duniani kuwakutanisha wanawake, vijana na makundi maalumu yaani watu wenye ulemavu ili kuwapatia elimu ya mikopo kutoka katika taasisi za kifedha” alisema Afsa Maendeleo ya Jamii Bi Neema.

Afsa Maendeleo ya Jamii Bi Neema Solomon akizungumzia kuelekea siku ya wanawake

Bi Neema amesema kuwa katika jamii bado wanawake wanakumbana na changamoto za ukatili hivyo wanashirikiana na Ustawi wa Jamii na taasisi ya Palaregal katika kutoa elimu ya kutambua ukatili na kuepukana na mila na desturi ambazo ni chanzo cha ukatili.

Afsa Maendeleo ya Jamii Bi Neema Solomon akielezea namna mila na desturi zinavyochangia ukatili katika jamii

Naye Makamu Mwenyekiti wa Paralegal Kilosa Bi Vimwaya Rashid Manyoli ambaye ni msaidizi wa kisheria amewataka wanawake kuachana na mila na desturi ili waweze kupaza sauti pindi wanapofanyiwa matendo ya kikatili ili sheria ziweze kuchukua mkondo wake.

Msaidizi wa kisheria Bi Vimwaya Manyoli akizungumzia namna ofisi ya Kilosa Paralegal inavyotoa elimu kwa wanawake

Hata hivyo Bi Vimwaya amesema kuwa umasikini ndio chanzo za ukatili na wanawake ndio wahanga hivyo amewataka wanawake kuacha kuwa tegemezi katika familia wanatakiwa wajishughulishe na shughuli za ujasiriamali ili waweze kujikwamua katika mateso wanayoyapitia.

Msaidizi wa kisheria Bi Vimwaya Manyoli akitoa rai kwa wanawake kuacha kuwa tegemezi katika familia
Msaidizi wa kisheria Bi Vimwaya Manyoli akiwa ofisini kwake Kilosa Paralegal