Radio Jamii Kilosa

Migogoro ya ardhi wilayani Kilosa sasa basi

2 February 2023, 2:12 pm

Katibu Tawala wilaya ya Kilosa akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya sheria wilayani hapa. Picha na Salumu Juma

Kutokujua sheria kwa wananchi imeelezwa ndio chanzo cha migogoro ya ardhi ya kudumu katika wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro ambayo huchochea migogoro ya wakulima na wafugaji hali inayochangia punguza ukuaji wa shughuli za kiuchumi.

Na Asha Madohola

Halmashauri Ya Wilaya Ya Kilosa yatakiwa kuyakusimamia vema mabaraza ya kijiji na kata ambapo migogoro ya ardhi ndipo inapoanzia na kuleta madhara makubwa kwa wananchi hususan wakulima huku mahakimu wakitakiwa kutoa elimu ya kisheria kwa wananchi.

Hayo yalisemwa Februari Mosi mwaka huu na Katibu Tawala Wilaya Ya Kilosa Yohana Kasitila katika Maadhimisho Ya Siku Ya Sheria ambayo yalifanyika katika viwanja vya Mahakama Ya Wilaya ya Kilosa ambapo alisema pia sababu nyingine ambayo inachangia ni halmshauri kushindwa kuyasimamia vizuri mabaraza ya kijiji na kata.

“Imefika mahali wananchi wilayani hapa wanachukulia migogoro ya ardhi ni sehemu yao ya maisha ya kawaida alisema katibu tawala kasitila”.

Sauti ya Katibu Tawala akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya sheria

Hata hivyo amevitaka vyombo vya mahakama vitende haki kwa kufuata sheria na maadili ya kazi ili kupunguza malalamiko kutoka kwa wananchi ambao mara nyingi wanakimbilia ofisi ya mkuu wa wilaya kutafuta masaada wa changamoto zinazowakabili.