Radio Jamii Kilosa

Epuka uchafu wa Mazingira Kilosa -M/kiti Chabu.

30 January 2022, 1:51 pm

Mwenyekiti wa Kilosa Jogging Club Hemedi Chabu akiwa Hospitali ya Wilaya Kilosa kwa ajili ya kufanya usafi

Wito umetolewa kwa jamii Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro kujenga tabia ya kushiriki kufanya usafi wa Mazingira na kupanda miti kwa ajili ya kuepuka magojwa ya mlipuko na kutunza Mazingira Wilayani humo .

Wito huo umetolewa Januari 29 mwaka huu na Mwenyekiti wa Kilosa Jogging Club Hemedi Chabu ,walipokuwa wakifanya usafi katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya Kilosa ikiwa ni moja ya utaratibu zao katika Klabu hiyo baada ya Kumaliza mazoezi ya viungo kushiriki shughuli za kijamii Kwa mujibu wa katiba kulingana na ratiba.

Katibu wa Kilosa Jogging Club Nora Shoo akifanya usafi katika Moja ya Wodi Hospitali ya Wilaya Kilosa .

Chabu amesema kuwa wameamua kufanya usafi katika Hospitali hiyo ni kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za serikali kwamba kila Jumamosi ya mwisho wa Mwezi ni siku ya usafi wa Mazingira hivyo Januari 29 2022 wamefanya usafi wa was Mazingira kwa kufyeka Nyasi, Kufagia na kupiga deki katika baadhi ya wodi .

Amesema kuwa Hospitali ni taasisi muhimu ambayo ilalazimika kuwa safi katika maeneo yote ndani na nje mazingira kwa ujumla kulingama na uwalisia wa huduma inayopatikana eneo hilo.

Wanajogging wakifyeka nyasi zilizo zunguka majengo ya Hospitali ya Wilaya Kilosa.

Hata hivyo Chabu amempongeza Muheshimiwa Mkuu wa Wilaya Kilosa Majidi Mwanga kwa kutoa wazo la kutaka kila kata kuanzisha Klabu ya mbio za mwendo pole almaarufu mchamchaka ili ziweze kuhamasisha maswala ya Afya ,Uchumi na Michezo na kubainisha kuwa Kwa sasa Kilosa Jogging Club ambayo ndio Klabu mama yenya makao makuu Kata ya Mkwatani,washa tembelea Klabu ya Kimamba Jogging Club iliyoko Kata ya Kimamba , Dumila Jogging Club ya kata ya Dumila na Kilombero Jogging Club ilioko Kata ya Ruaha ambapo ameziomba Kata zingine kuhamasika kuanzisha Klabu zao ambazo zitasaidia kuhamasisha wananchi kujitoa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii ,Michezo na Uchumi na kwamba Jamii ya watu wa Kilosa inatakiwa kutambua ukitengeneza Mazingira yatakutuza pamoja na kizazi kijacho.

Afisa Afya wa Hospitali ya Wilaya Killosa Ahobokile David .

Naye Afisa Afya wa Hospitali ya Wilaya Kilosa Ahobokile David amewashukuru Kilosa Jogging Club kwa kazi waliyo ifanya kwani Mazingira yalikuwa ni machafu kutokana na kukua kwa nyasi kuzunguka majengo kuliko sababishwa na mvua zinazo endelea kunyesha.

Amesema kuwa Mazingira yanapokuwa machafu kunaweza kusababisha kuvamiwa na wadudu hatari watambaao kama vile Nyoka, kupata magonjwa ya mlipuko ambapo amewaomba wanajogging kuwa na moyo huo wa kujitolea na kuitaka jamii na taasisi zingine kuiga mfano wa Klabu hiyo kwani Afya ya binadamu hutengenezwa na Mazingira.