Radio Jamii Kilosa

Tubadirike Magufuli kurudi Kilosa hatopita barabara wala Reli ya mwendokasi .

21 March 2021, 11:39 am

Waamini wakatoriki wa Parokia ya familia takatifu Kilosa wakiwa ndani ya kanisa wakisikiliza neno la Mungu.

Waumini wa Romani katoliki parokia ya familia takatifu Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro wametakiwa kubadirika ndani ya mioyo yao na kumrudia Mungu hasa kipindi hiki cha kwaresma kwa kufunga Kulia na kuomboleza kwakuwa hakuna anaejua siku wala saa ya kifo chake na kwamba kufanya hivyo Mungu atawapa nguvu ya kupambana na changamoto za maisha hapa Duniani.

Mwalimu wa Semina ya Kiroho katika Parokia ya familia takatifu Kilosa Regina Masalu akitoa neno kwa waamini.

Hayo yamesemwa machi 21, 2021 na Mwalimu wa Semina ya kiroho Regina Masalu alipo kuwa katika ibada ya jumapili baada ya kupata nafasi ya kuwahutubia waamini wa kanisa hilo ambapo amesema kuwa Mungu bado anatoa nafasi ya kubadirika kiroho kwa sababu wakati wowote usio tarajiwa anaweza kukuita kwake kwaiyo ni muhimu kufanya toba ya kweli kwa kufunga, Kulia na kuomboleza ,kusamehe huku ukijua unahitaji kubadirisha maisha.

Amesema kuwa hayati Rais John Pombe Magufuli mwaka 2020 alifika Wilayani Kilosa kwa ajili ya kukagua Miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na Ujenzi wa Reli ya mwendo kasi SGR na Barabara ya Rudewa kwenda Kilosa Mjini zaidi ya kilometa 20 inayojengwa kwa kiwango cha lami ambapo aliahidi wananchi wa Kilosa kuwa atarudi tena kuona mandeleo ya Miradi hiyo.

Waamini wakatoriki Kiosa wakisikiliza neno la Mungu

Masalu amesema kuwa Rais Magufuli sasa hatopita Barabara hiyo, hatopita Reli ya mwendo kasi na hatoiyona Treni ya Mwendo kasi tena kwakuwa mwenyezi Mungu amemchukuwa tukiwa bado tunamuhitaji hivyo ni pigo kubwa kwa waamini wa Kilosa na taifa kwa ujumla na kwamba kupitia kifo chake ni funzo kwa watu wengine na ni wakati wa kutafakali kuwa wewe ni nani mbaka kushindwa kufanya maamuzi Sasa, kumrudia Mungu mana kunawengine bado wanawaza kumrudia Mungu kwaresma ya mwakani na wengine kuitaji kuishi katika maisha ya dhambi na wengine wakisubiri badae wakati hakuna anayeifahamu badaye .

Masalu amesema kuwa tupo katika wakati mgumu kwani Jamii imekuwa ikiishi katika changamoto mbalimbali za kiuchumi, kikazi, kimaadili hasa vijana wanavyo vaa na kunyoa, changamoto kwa watoto, ndugu na marafiki hivyo kila mtu kwa nafasi yake anapaswa kumrudia Mungu ili aweze kumpa nguvu za kupambana na changamoto za maisha.