Radio Jamii Kilosa

Zaidi ya wanafunzi 2700 kupewa elimu ya Kinywa Kilosa -Dk Kibula.

17 March 2021, 11:57 am

Mratibu wa afya ya kinywa na meno Wilaya ya Kilosa Dokta Thomas Kibula akiwa katika mahojiano Radio Jamii Kilosa

Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro kupitia idara ya afya wanatarajia kutoa elimu ya afya ya Kinywa na meno pamoja na vifaa vya kushafishia Kinywa kwa wanafuzi 2721 kwa ajili ya kujikinga na magonjwa mbalimbali ya Kimywa na meno.

Hayo yamesemwa machi 17 2021 na Mratibu wa kinywa na meno Wilaya ya Kilosa Dokta Thomasi Kibula alipokuwa akifanya mahojiano katika kipindi cha Mambo mseto kinachorushwa na Radio Jamii Kilosa kuhusu wiki ya maadhimisho ya afya ya Kimywa na meno ambayo huanzia tarehe 15 machi hadi tarehe 20 machi kila mwaka .

Dk Kibula amesema katika kuadhimisha wiki ya Afya ya kinywa na meno mwaka huu idara ya afya wilaya ya Kilosa kwa kushilikiana na Timu ya usimamizi wa huduma za afya Mkoa RHMT licha ya kutoa elimu kwa wanafunzi wa Shule za msingi Mazinyungu, Kilosa town,Manzese ,Kichangani na Madaraka zenye jumla ya wanafunzi 2721 pia watawapatia wanafunzi wenye mahitaji maalumu wa shule ya msingi Mazinyungu vifaa vya kushafishia Kinywa Kama vile Dawa za meno na Miswaki.

Amesema kuwa lengo la kutoa elemu kwa wanafunzi kwanza ni mabarozi wazuri katika kufikisha ujunbe kwa wazazi wao na jamii kwa ujumla pili ni kuwajengea uwezo wa kusafisha vinywa vyao kwa usahihi ili kujikinga na magonjwa yasiweze kushambulia Kinywa kwa urahisi kwani wao ndio wako katika umri wa kuota meno ya ukubwani ili yasiweze kupata madhara Kama vile jino kutoboka, fizi kutoa damu,na harufu mbaya kutoka kinywani.

Dk Kibura mratibu wa afya ya kinywa na meno Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro

Sambamba na hayo Dk Kibula amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya kilosa bado inachangamoto kubwa ya utoaji huduma za afya ya kinywa na meno kwani vituo vyote vya afya vya serikali zikiwemo zahanati havitoi huduma hiyo kwakuwa hakuna wataalamu wa Kinywa na mano hivyo wananchi hulazimika kutembea umbali mrefu kupata huduma katika hospitali ya Wilaya.

Kibula amesema kuwa hospital ya Wilaya pia ina dakta mmoja ambaye anapokea wagonjwa Kati ya 90 hadi 100 kwa mwezi ambapo bado ni mzigo mkubwa katika kutoa huduma vivyo kuna haja ya kupeleka wataalamu wa Kinywa na meno katika zahanati na vituo vya afya vya serikali ili kuwapunguzia safari wananchi.

Wiki ya Afya ya Kinywa na meno huadhimishwa kila mwaka ifikapo machi 15 na kilele chake ni Machi 20 ambapo kaulimbiu ya mwaka huu ni “Jivunie kinywa chako”