Radio Jamii Kilosa

Bilion 1.27 kumaliza tatizo la maji kilosa-Injinia Chum.

16 March 2021, 11:44 am

Meneja wa Ruwasa Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro Injinia Josho Hamisi Chum akiwa katika mahojiano Radio Jamii Kilosa.

Zaidi ya bilion 1.27 zimetengwa kwa ajili ya miradi ya maji  safi na salama Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro ili wananchi waweze kupata huduma ya maji  saa 24  kwa mwaka .

Hayo yamesemwa machi 16 2021 na Meneja  wakala wa maji na usafi wa mazingira Ruwasa Wilayani kilosa Injinia   Joshi Hamisi  Chum alipokuwa katika kipindi cha mambo mseto kinachorushwa na Radio  Jamii Kilosa wakati akizungumzia wiki  ya  maji ambayo huazimishwa kuanzi tarehe 16 machi hadi 22 machi kila mwaka.

Meneja Ruwasa Kilosa Injinia Joshi Chum

 Chum amesema kuwa Halmashauri imetenga kiasi cha shilingi bilioni  1,270,000,000 kwa mwaka wa fedha 2020/2021 kwa ajili ya kumalizia miradi iliyopo  katika vijiji mbalimbali wilayani humo ikiwa ni pamoja na kuanzisha miradi mipya sehemu ambako bado kunachangamoto ya upatikanaji wa maji na kueleza kuwa kwasasa Ruwasa imefanikiwa kusamabazamaji kwa asilimia 73 kwa upande wa  vijiji na  mijini asilimia 85

Amesema kuwa ,kuna baadhi ya vijiji vinachangamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na vyanzo vya mazi kukauka, kutokana na shughuli  za kibinadamu  kama vile kilimo na uchimbaji wa madini  ambapo  tayali wameshaanza kufanya utafiti wa kubaini maeneo  katika vijiji  ambavyo havina maji safi na salama   ili kuaza kuchimba visima virefu vitakavyo sambaza maji katika katika maene yapo .

Chum amefafanua kuwa   maadhimisho  wiki ya maji duniani kwa wilaya ya Kilosa  itaadhimishwa kwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja  na kuzindua mradi wa maji Belega,kukagua uchafuzi wa vyanzo vya maji kata ya Ruaha,kukagua miradi ya maji inayo endelea maeneo ya , Kitete,Dumila,Mabwegere, kuhamashisha wananchi kutunza mazingira  pamoja na kupokea changamoto za upatikanaji wa maji katika kijiji cha Tindiga .

Hata hivyo amesema kuwa kunabaadhi ya vyanzo vya maji vilivyokuwa vinasambaza maji katika mji wa Kilosa vimeharibika kutokana na mafuriko ya mto mkondoa  ambavyo ni  Nguzo sita na  Mkondoa hali inayopelekea kuwa na changamoto ya kupatikana kwa maji katika baadhi ya maeneo na kusababisha mgawo  wa mji na kuongeza kuwa jitihada zinafanika ili kubaini vyanzo vingine   kumaliza tatizo hilo la mgao .