Radio Jamii Kilosa

Takukuru yaokoa shilingi milioni 8.3 Kilosa.

14 January 2021, 2:31 pm

Mkuu wa takukuru Wilaya ya Kilosa Lawrence Mlapon akiwa Ofisini kwake akizungumza na Waandishi wa Habari Kilosa.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro imefanikiwa kuokoa fedha kiasi cha shilingi milioni 8,300,000 Kati ya milioni 212,503,559.29 ambazo chama cha Ushirika wa Akiba na mikopo cha Walimu Wilayani humo (Kilosa Teachers Saccos) kinadai wanachama wake ambao ni wadaiwa sugu waliokopa na kushindwa kurejesha kwa muda mrefu.

Akitoa Taarifa kwa Waandishi wa Habari Kilosa Januari 14 Mwaka huu Mkuu wa Takukuru Wilaya ya Kilosa Lawrence Mlaponi amesema kuwa Chama hicho Kilosa Teachers Saccos kilisajiliwa kwa mujibu wa sheria ya vyama vya Ushirika na kupata cheti cha usajili N0 .MGR.240 tarehe 02/7/1999.

Kwa mujibubwa taarifa aliyo itoa Chama hicho kilikuwa na wanachama waanzilishi 190 hadi kufikia Desemba 2012 Chama kilikuwa na wanachama 1,160 ambao ni walimu wanaotoka Idara za Elimi Msingi na Sekondari wanaofanya kazi Katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa na kwamba Chama hicho kilikuwa na changamoto mbali mbali za kiuwendeshaji toka mwaka 2009 zilizo sababisha wanachama wengi kukosa huduma kwa wakati ,kushindwa kulipa madeni bank,kulipa Akiba, Amana na hata Hisa za wanachama pale wanapo lazimika kurejesha fedha hizo.

Aidha kutokana na changamoto hizo Takukuru Kilosa ilianza kufuatilia madeni hayo ya wanachama wa Kilosa Teachers Saccos toka mwaka 2019 ambapo Chama kilikuwa kinadai Jumla ya kiasi cha zaidi ya Shilingi milioni 212 na kwamba takukuru imefanikiwa kurejesha kiasi cha shilingi milioni 8.3 kutoka kwa wanachama wadaiwa sugu 30 na kuongeza kuwa Takukuru Kilosa inaendelea kuwafuatilia wadaiwa wengine sugu hata wale walihama kuhakikisha wanarejesha fedha hizo.

Kwaunde wake Mjumbe wa bodi ya Kilosa Teachers Saccos Bw Issah Nyamkunga ameishukuru Taasisi hiyo kwa kazi nzuri waliyo ifanya kwani wadaiwa hao sugu wamekuwa wakisumbua pindi wanapowafuata ili waweze kulipa madeni yao.