Radio Jamii Kilosa

Kilosa yajipanga kuto poteza vipindi darasani.

14 January 2021, 2:55 am

Mkuu wa shule ya Sekondari Mazinyungu Ngamba Manegese akiwa Darasa anafundisha

Wakati shule zikifunguliwa kwa ajili ya wanafunzi kuanza rasmi masomo yao Januari 11 mwaka huu mkoa wa Morogoro upande wa elimu sekondari umejipanga kuishi katika kauli mbiu ya hakuna kipindi kupotea lengo likiwa ni kuhakikisha wanafunzi wanafaulu katika kiwango kizuri kinachoridhisha.

Hayo yamebainishwa hivi karibuni na Mkuu wa shule ya Sekondari Mazinyungu Ngamba Manegese ambapo amesema licha ya mkoa wa Morogoro kuishi katika kauli hiyo halikadhalika Wilaya ya Kilosa itasimamia kauli hiyo kwa kushirikisha walimu, wazazi na wanafunzi kwani mwanafunzi hawezi kuwa na ufaulu mzuri endapo hatashiriki vizuri katika vipindi hivyo .

Akizungumzia upande wa shule ya Sekondari Mazinyungu amesema wamejipanga kuhakikisha ufaulu wa watoto unakuwa mzuri kwa kuwa na ushirikiano mzuri baina ya wazazi, walimu na wanafunzi pamoja na uwepo wa mitihani ya mara kwa mara huku akimshukuru Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji na uongozi mzima wa Idara ya Elimu Sekondari kwa namna ambavyo wamekuwa wakitoa ushirikiano wa kutosha ili kufikia malengo.

Ngamba amesema kwa upande wa kidato cha nne wamejipanga kuhakikisha mada zote zinakamilika ifikapo mwezi Mei ili kuwa na muda mzuri na wakutosha kea ajili ya kufanya marudio jambo litakalowasaidia walimu kuwasaidia wanafunzi maeneo yenye changamoto jambo litakalopelekea kuleta matokeo chanya.

Akiongea kwa niaba ya wanafunzi wenzake wa kidato cha nne Happiness Msafiri a kuwa wamejipanga vizuri kuhakikisha kiwango cha taaluma na ufaulu kinakuwa vizuri ikiwemo kuwa na vikundi vya kujisomea, kuweka kambi ya kidato cha nne shuleni hapo ili kuwa na jambo muda mzuri wa kujisomea .