Radio Jamii Kilosa

Wakina Mama wanao Nyonyesha watakiwa kuzingatia usafi wa Mwili na Mazingira- Kilosa.

8 January 2021, 10:26 am

Mratibu wa shughuli za wahudumu kutoka katika Mradi wa Lishe Endelevu Kilosa Bwana Revocatus Mussa akiwa Katika mahojiano na radio Jamii kilosa.

Wakinamama wanao nyonyesha watoto walio chini ya siku 1000 toka kuzaliwa wameshauriwa kuzingatia usafi wa mwili na Mazingira wakati wa kunyonyesha na kuandaa Chakula cha ziada kwa mtoto aliye fika umri wa miezi sita.

Akizungumza na Radio Jamii Kilosa katika kipindi cha Mambo mseto Januari 8 ,2021 Mratibu wa Shughuli za wahudumu kutoka Mradi wa Lishe Endelevu Wilayani Kilosa Revocatus Mussa amesema Usafi wa mwili ni muhimu sana kwani utasaidia kumuepusha mtoto kunyonya uchafu hasa jasho ambalo linaweza kusababisha kupata magonjwa mbali mbali ya tumbo na Kuharisha.

Amesema kuwa Mtoto aliye chini ya siku 1000 hana ufahamu wa kutambua vyakula vinavyoweza kumleta madhara hivyo wakinamama wanapoandaa Chakula cha ziada cha mtoto ni nimuhimu kuandaa mazingira mazuri ya Chakula kwa kusafisha vifaa vitakavyo tumika ili kuepuka uchafu ambao unaweza kuleta madhara kwa Mtoto.

Aidha Mussa amesema ni vizuri kumpa mtoto Chakula cha ziada akiwa ametimiza umri wa miezi sita kwani umri huo unafaa kuanza kupatiwa Chakula laini ambacho kutakuwa kimesagwa au kutafuna ili iwe rahisi kumeza ambacho hakitaweza kumletea matatizo kwani mfumowake wa kumeng’enya Chakula bado hauja komaa .

Hata hivyo ameongeza kuwa Chakula cha ziada ni muhimu kikaandaliwa kwa kuzingatia makundi matano ya Chakula ambacho kitamsaidioa kujenga Mwili Afya, na akili.