Radio Jamii Kilosa

Wananchi wametakiwa kupanda Miti,Maua na kusafisha Mifereji ya Maji ya Mvua -Kilosa.

7 January 2021, 2:39 am

Mfereji unao tiririsha maji kutoka eneo la Uwindini kuelekea Mtoni Mkondoa Mjini Kilosa

Wananchi Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro wahamasishwa kupanda Miti na Maua pamoja na kusafisha Mifereji ya Maji ya Mvua Ili kutunza Mazingira.

Afisa Mazingira Kilosa Anthony Heriel Mbise akifanya mahojiano Katika kipindi cha usafi na Mazingira Radio Jamii Kilosa .

Akizungumza na Radio Jamii Kilosa Januari 6,2021 Afisa Mazingira Kilosa Anthony Heriel Mbise kuwa ni vizuri Wananchi wakatumia Mvua zinazo endelea kunyesha kupanda Miti na Maua.

Amesema kuwa Maua yanasaidia kupendezesha Mazingira ya eneo husika pia Miti inasaidia kupatikana kwa hewa safi na kupunguza hewa ya ukaa (carbon dioxide), inasaidia kupunguza madhara yatokanayo na upepo unaovuma kwa kasi pamoja na Mmomonyoko wa Udongo.

Mbise amesema kuw kusafisha Mifereji kutasaidia maji ya Mvua kutiririka Katika miundombinu iliyojengwa pasipo kuingia kwenye makazi ya watu na kutuama ambayo yatasababisha kuwa na mazalia ya Mbu.

Aidha amesema Mifereji ikiwa Michafu kutasababisha maji kutiririka juu ya Mifereji hiyo na kuharibu miundombinu ya Barabara jambo litakalo pelekea Serikali kuingia Gharama za ukarabati.