Radio Jamii Kilosa

Wananchi Wilayani Kilosa Wametakiwa kutunza na kuifadhi mazingira .

6 January 2021, 3:10 pm

Wananchi Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro wahamasishwa kupanda Miti na Maua pamoja na kusafisha mifereji ya maji ya mvua Katika maeneo yao Ili Kutunza mazingira.

Afisa Mazingira Kilosa Bwana Anthony Heriel Mbise akifanya mahojiano na Radio Jamii Kilosa Katika kipindi cha usafi na mazingira .
Ni moja ya mfereji unaotiririsha maji ya mvua kutoka eneo la Uwindi kuelewa Mto Mkondoa kilosa.

Akizungumza na Radio Jamii Kilosa januari 6,2021 Afisa Mazingira Kilosa Anthony Mbise amesema kuwa ni vizuri wananchi wakatumia Mvua zinazoendelea kunyesha kupanda miti na maua.

Amesema kuwa maua yanasaidia kupendezesha mazingira yanayo zunguuka eneo husika ambapo Miti inasaidia kupatikana kwa hewa Safi, na inazuia madhara yatokanayo na upepo unaovuma kwa kasi,kupunguza hewa ya ukaa (carbon dioxide),pamoja na Mmomonyoko wa udongo .

Mbise amesema kuwa, kusafisha Mifereji kutasaidia Maji kutiririka katika miundombinu iliyo jengwa na pia itasaidia maji kuto ingia kwenye makazi ya watu na kutuama ambayo yatasababisha mazalia ya Mbu.

Aidha amesema maji yatakapo pita juu ya mifereji yanaweza kuleta athali kubwa za kimazingira ikiwa ni pamoja na kuharibika kwa miundombinu ya barabara jambo litakalo pelekea serikali kuingia gharama za ukarabati.