Radio Fadhila

Door of Hope wakutana na vijana, wawapa mbinu za utambuzi

8 June 2023, 9:55 AM

Shirika lisilo la kiserikali la DOOR OF HOPE lenye makao yake mkoani Mtwara limekutana na vijana  zaidi ya 30 kutoka  kata za Jida na Migongo  ili kuwajengea uwezo wa utambuzi katika mradi wa Kijana Kwanza ambao unatekelezwa katika halmashauri ya mji wa Masasi.

Akizungumza katika warsha hiyo ya siku mbili mwezeshaji  kutoka shirika hilo Jesca Mhagama ametumia nafasi hiyo kuwataka vijana kuwa na chaguzi sahihi za marafiki kwani kuna baadhi ya marafiki wapo kwa ajili ya maslai tu kwa kusema

Katika warsha hiyo ya siku mbili pamoja na mambo mengine imelenga kuwajengea uwezo vijana katika ushiriki chanya katika masuala ya utawala bora pamoja na serikali za mitaa.