Radio Fadhila

Mkurugenzi MTWANGONET Mtwara ahimiza jamii kupunguza vitendo vya kikatili

29 May 2023, 9:54 AM

MASASI

Ili kutokomeza vitendo vya ukatili katika jamii , mkurugenzi wa asasi isiyo ya kiserikali kutoka mkoa wa Mtwara MTWANGONET, Fidea Luanda amesema ni wajibu wa kila mmoja katika katika jamii ukatimiaza majukumu yake ili kupunguza vitendo vya kikatili.

Fidea  ametoa ushauri huo wakati akifanyiwa mahojiano na Radio Fadhila katika kipindi maalum kilicholenga kutoa fursa kwa asasi hiyo kueleza utafiti uliofanywa na asasi hiyo kwa Vijana nchi nzima wenye umri wa miaka 13-17 uliobaini changamoto mbalimbali kwa vijana ikiwemo kushuka kwa maadili katika kundi hilo.

Katika mradi huo wa upimaji Taasisi hiyo imewezeshwa na Regional, Education, Learning, Initiative RELI, Milele Zanzibar Foundation na Uwezo.

Utafiti huo ambao umefanyika nchi nzima huku mkoa wa Mtwara ukihusisha wiilaya ya Masasi umebaini changamoto mbalimbali kwa vijana ikiwemo kushuka kwa maadili, kutokuwepo ushirikiano wa kutosha  baina ya vijana, ufinyu wa uelewa wa  utatuzi wa matatizo yao, na uelewa duni wa matumizi ya teknolojia simu.

Fidea akizungmza katika sehemu ya wasilisho lake akasema…