Radio Fadhila

Mtandao wa Askari wanawake Tanzania na watoto wenye usonji

9 March 2023, 11:04 AM

Askari wanawake na watoto wenye uhitaji

Picha na Lilian Martin

Katika kilele Cha siku ya wanawake Duniani umoja wa Majeshi wilayani Masasi kupitia mtandao wa Askari wanawake wameadhimisha siku ya wanawake Duniani Kwa kuwa pamoja na watoto wenye mtindio wa ubongo na usonji katika shule ya watoto wenye mahitaji maalumu Lulindi na kujumuika pamoja nao.

umoja huo wa Majeshi wilayani Masasi uliwapatia watoto hao vitu mbali mbali ikiwemo Magodoro,Neti,sabuni,juice biscuit,viatu unga pamoja na Mafuta ili kufurahi pamoja nao na kutambua uwepo wa watoto hao katika jamii

Askari akikabidhi juice mwanafunzi

Na kwa upande wake Afande mkuu wa upelelezi wilaya ya Masasi Christopher Msonsa ambaye pia ni mkuu wa msafara huo amesema kuwa anatambua juhudu za wanawake

“Nimeongozana na Amsafara huu ikiwa ni siku ya wanawake Duniani Kwa maana natambua jitihada za wanawake kama wamama na walezi wazuri wa famili hivyo niwazi kuwa nawaunga mkono Kwa kufurahi pamoja na watoto Hawa”

Akizungumza mkuu wa msafara