Radio Fadhila

Mbunge awapongeza Kwa ubunifu week ya elimu Masasi

3 March 2023, 9:43 PM

Wanafunzi wakigumbuiza Kwa ngoma

katika siku ya maadhimisho ya week ya elimu Kwa Halmashauri ya mji Masasi yaliyohudhuriwa na wanafunzi wa shule za msingi na secondary zilizopo katika halmashauri hiyo pichani ni wanafunzi wakionyesha burudani.

sambamba na hayo katika maadhimisho hayo yaliyohudhuriwa na Mh Jophrey Mwambe Mbunge wa Masasi alitembelea katika vibanda na kuangalia ubunifua wa waalimu katika halmashauri hiyo na kuonyesha zana zao za kufundishia

Mwalimu alielezea zana za kufundishia

“Tunatumia vitu mbalimbali ili kutengeneza zana ambazo wanafunzi anakuwa namu ya kujifunza zaidi kama huu mti unakaa darasani na timebandika maneno mbalimbali hivyo mtoto anaanza kuvutiwa na mti na baadae kulazimika kujifunza maneno ya kweny huu mti”.

Mbinu za kufundishia

“wakati mwingine vifaa vya kutengenezea maneno ni gharama kununua bidhaa dukani hivyo basi tunabuni njia mbadala ndiyo tunatumia vitu vya asili kama upupu mbaazi nk ili kuandikia maneno ambayo yatasaidia hata Kwa watoto wenye changamoto ya kuona kama kutumia nucta nundu”alisema Mwalimu huyo