Radio Fadhila

Wanafunzi Shule ya Msingi Migongo wapatiwa Elimu ya Usalama Barabarani.

17 February 2023, 11:00 AM

Masasi Kamati ya Usalama Barabarani kitengo cha elimu, mafunzo na uenezi  kwa umma kimeendelea kutoa elimu katika makundi mbalimbali ya Wilaya hiyo, ambapo mapema wiki hii imetoa elimu Shule ya Msingi migongo Wilayani Masasi Mkoani Mtwara.

Akizungumza katika kutoa elimu  mjumbe wa kamati hiyo CLP. RODRIQUE MWANGUNGULU, kutoka Kituo cha Polisi Masasi amewasisitiza Wanafunzi kueshimu sheria za Usalama Barabarani na kujiepusha kuvuka barabarani pale wanapoona kuna Magari ya dharura na misafara Inapita.

Aidha katika atua nyingine Mwangungulu ametoa rai kwa Wanafunzi wa Shule ya Msingi Migongo kuwa Mabalozi wa zuri kwa wengine ambao hawajapata elimu ya usalama Barabarani ili kuepukana na ajali za barabarani ambazo wakati mwingine zinasababishwa na uzembe wa kutozingatia sheria hizo.