Radio Fadhila

Usalama wa mwanafunzi katika kufikia mpango wa shule salama

3 February 2023, 3:49 PM

Kikao Cha wazazi na walimu kutekeleza mpango shule salama

Walimu wa Shule ya Sekondari Masasi Kutwa, iliyopo Wilayani Masasi, Mkoani Mtwara wamewataka wazazi na walezi kuwa walinzi wa kwanza Kwa watoto wao wanaporudi nyumbani kutoka shuleni ili kufikia lengo la kutekeleza mpango wa shule salama

Kwa upande wake Mwalimu Anatoli amewataka wazazi kuwa macho na watoto wanaporudi nyumbani na kuimarisha ushirikiano baina ya mzazi na mwalimu ili kutatua changamoto za watoto Kwa pamoja na kufikia lengo la shule salama

“Ili kufikia lengo la shule salama ni lazima kuwe na ushirikiano baina mazazi na mwalimu kwani hii italeta hata matokeo mazuri kwa wanafunzi na atakuwa salama wakati wote awapo nyumbani na anapokuwa shuleni” amesema Mwalimu Anatoli