Radio Fadhila

Upendo Charity yaguswa na tatizo la Salma

30 January 2023, 4:17 PM

Kikundi kinachosaidia watu wenye uhitaji kilichopo Wilayani Masasi,Mkoani Mtwara, kinachofahamika kama Upendo Charity kimeguswa na tatizo la mtoto Salma Pascha Machemba, mwenye umri wa miaka tisa (9) ambaye anaishi Kijiji cha Matekwe Majenanga, huko Nachingwea Vijijini.

Salma ni mlemavu wa viungo ambaye pia alipata ajali ya kuvunjika miguu yake ambayo na hana usaidizi kwani anatumia makalio kutoka sehemu moja hadi nyingine

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kikundi cha upendo charity Bi. Chiristina Simo amemtembelea mtoto Salma katika Hospital ya Ndanda ambako anapata matibabu na kumpatia baadhi ya vifaa vya shule ili kumsaidia katika masomo yake

Aidha Bi. Simo ameiomba jamii kujitoa kuwasaidia watu wenye uhitaji katika jamii ili nao wajisikie faraja kwa hali waliyonayo

Mtoto Salma akiwa na madam simo