Radio Fadhila

Shule ya Msingi Mkuti B yapata Viongozi wapya

30 January 2023, 12:31 PM

Shule ya Msingi Mkuti “B” Wilayani Masasi, imefanya Mkutano wake Mkuu wa Kwanza wa Shule hiyo na kuwachaguwa viongozi mbalimbali wa shule pamoja na kujadili ajenda za mipango ya maendeleo ya shule.

Mkutano huo ambao umefanyika Shuleni hapo mapema wiki hii, viongozi waliochaguliwa wa Bodi ya Shule ni Mwenyekiti pamoja na Wajumbe watatu waliopita bila ya kupingwa baada ya mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti kujitoa katika kinyang’anyiro na wajumbe kupita bila kupingwa

Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwanahabari wetu mara baada ya kuitimishwa kwa Mkutano huo, Mwenyekiti aliyechaguliwa, Salumu Katondo, ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Shule ya Mkuti kabla ya kutenganishwa amewashukuru wananchi kwa juhudi zao

Aidha Mkuu wa Shule, Nurdin Mussa Mnanga, akizungumza na mwandishi wetu amewataka wazazi na wadau waliotoa ahadi ya kuchangia ujenzi wa vyoo vya walimu watoe kwa wakati

Wakati huo huo Wazazi walioshiriki Mkutano huo wakatumia fursa hiyo kuhamasishana kutoa michango kwa wakati kama sehemu ya kushiriki ujenzi huo

Mkuu wa Shule ya Msingi Mkuti B Nurdin Mnanga akizungumza na wananchi

Kwa upande wake Mdau wa Malezi ya Watoto, ambae pia ni Mwenyekiti wa Kikundi cha Upendo Charity, Christina Simo, akizungumza katika Mkutano huo amewasisitiza wazazi kuwafuatilia wanafunzi katika suala la malezi pamoja na masomo

Mdau wa Malezi ya Watoto Bi. Christina Simo akiongea kwenye Mkutano huo