Radio Fadhila

Shule jumuishi Ya Mfano Ya Msingi Lukuledi Imeziduliwa!!!

16 January 2023, 10:07 AM

MASASI.

Waziri wa Elimu Profesa Adolf   Mkenda amezindua  Shule ya Msingi jumuishi ya mfano Lukuledi Wilayani Masasi mkoani mtwara ikiwa ndio shule ya kwanza ya mfano kwasasa ambayo huwezi kuiona sehemu nyingine  Tanzani kwa ukubwa na wingi wa miundombinu  huku akitoa pongezi kwa Mashirika yaliyowezesha ujenzi huo kukamilika  kwake ambayo ni UNESCO,UNICEF na BANK YA DUNIA.

Shule hiyo ambayo inapokea Wanafunzi  wenye ulemavu wa viungo na wale ambao wanaulemavu wa kutosikia Viziwi imejengwa kwa gharama ya Shilingi bilioni I.5, huku ikiwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi  480 kwa mkupuo mmoja.

 

Profesa Mkenda  wakati akizundua shule hiyo ametumia nafasi hiyo kusisitiza jamii kutowafungia watoto wenye mahitaji maalumu badala yake wawapeleke  shuleni kwani Raisi Samia  Suluhu Hasani alishatoa agizo  Watoto wote wapelekwe  Shuleni na hasiachwe mtoto  kwa sababu ya tatizo la ulemavu au kupata ujauzito wote wapatiwe fursa ya kusoma na ndio maana Serikali inajenga Shule kama hizo.

Aidha kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Chama Mapinduzi CCM, Wilayani Masasi Mariamu Kasembe akatumia nafasi hiyo kuiyomba Serikali iweze kuwajengea uzio watoto hao kama sehemu ya kulinda usalama wa wao.

Shule hiyo kwa sasa inawanafunzi wapatao 145 huku Wasichana wakiwa 71 na Wavulana 74.

Shule hiyo inaofisi sita, madarasa kumi na mbili, bwalo lenye uwezo wa kuhudumia Wanafunzi mia tatu likiwa limeambatanishwa na Jiko na Stoo , Mabweni manne yenye uwezo wa kuchukuwa Wanafunzi 480 yakiwa na vyumba maaalumu, Nyumba za Walimu  tisa, na Jiko kwa ajili ya kupikia.