Radio Fadhila

CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA MASASI CHA MPONGEZA RAISI

10 January 2023, 2:27 PM

Katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi  wilaya ya masasi TWAHILI SAIDI MAYOLA, amezungumza na radio fadhila  juu ya tamko la raisi wa jumuhuri ya muungano wa Tanzania  dkt samia suluhu  hassan kuruhusiwa kwa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa nchini ,ni miaaka 6 sasa imepita tangia kufungiwa kwa vyama  vya siasa kufanya mikutano ya hadhara.

“Amesema wao kama chama cha mapinduz ( ccm) wamepokea kwa furaha kubwa tamko la raisi wa jamuhuri ya muungano wa tanzania” na wanampongeza raisi kuruhusu mikutano ya hadhara kwani wamejipanga kuwapa nafasi wananchi  na kuzungumzia yale yanapaswa kusemwa na wananchi pia wao kama chama kilicho shika dola watapata fulsa ,ya kusema yale mazuri yote yaliyo fanywa  na serikali ya chama cha mapinduzi kupitia ilani ya chama cha mapinduzi.

.