Radio Fadhila

Mkuu wa Wilaya Masasi amewataka wananchi kusherekea Sikukuu za Mwisho wa Mwaka kwa Amani

31 December 2022, 12:56 PM

Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Bi.  CLAUDIA KITTA, ametoa Rai kwa Wananchi wa Masasi katika kuelekea Sikukuu za Mwisho wa Mwaka za Krismasi na Mwaka Mpya kusherehekea kwa utulivu na amani.

Pia amesisitiza na kuwahimiza wazazi na walezi kuwalinda watoto ili kuwaepusha na madhara ikiwemo ya kupata ajali.

Bi. Kitta ametoa Rai hiyo wakati akifanyiwa Mahojiano Maalumu na Mwandishi wetu.

Aidha akizungumza wakati anatoa salamu za Krismasi na Mwaka Mpya

Pamoja na hayo Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wananchi Wilayani Masasi   kushiriki katika zoezi la Kilimo hasa mazao ya Chakula na Biashara kwa kasi kwa sababu mvua zimeanza kunyesha na  na hakuna sababu yeyote ya kuacha kulima kwani mbolea ruzuku na mbegu zipo

.