Radio Fadhila

Mbunge wa Jimbo la Ndanda, Cecil David Mwambe , ameshiriki hafla ya mapokezi ya Majengo Kwa ajili ya Shule ya Sekondari Mpanyani.

23 December 2022, 7:50 AM

Mbunge wa Jimbo la Ndanda, Cecil David Mwambe, ameshiriki hafla ya mapokezi ya Majengo Kwa ajili ya Shule ya Sekondari Mpanyani.


Majengo hayo yaligarimu sh 460m yamekamulika na tayari wanafunzi 160 waliochaguliwa kuingia kidato Cha kwanza wataanza kuyatumia Kuanzia January 2023.


Wananchi katika salamu Zao wameishukuru Sana Serekali ya Chama Cha Mapinduzi inayoongozwa na Mh Raisi Samia Suluhu Hassan Kwa kuwatatulia Kero hiyo na kuwapunguzia watoto umbali mrefu wa kutembea Kwa kufuata Shule kata za jirani.