Radio Fadhila

Waandishi wa Habari Radio Fadhila wapigwa Msasa

16 December 2022, 10:19 AM

Na Lawrence Kessy

Waandishi wa Habari wa Kituo cha Radio Fadhila wamepata mafunzo ya jinsi ya kuandaana kuchakata habari za Mitandao ya Kijamii pamoja na kuzingatia maadili ya tasnia ya habari

Mafunzo hayo yametolewa Alhamisi Desemba 15, 2022 na Amua Rushita kutoka IT Jamii FM, Mtwara pamoja na Markku Liukonen kutoka Vikes Finland, kwenye Ukumbi wa Radio Fadhila uliopo Kituoni hapo, Mjini Masasi, Wilayani Masasi, Mkoani Mtwara

Rushita amewashauri waandishi hao wasiwe na tabia au hali ya kuahirisha jambo kwani itakuwa ndiyo tabia na mwendelezo katika kazi zao na kuanza kujitengenezea mazoea ya kutojituma

Aidha, amewataka pia kuenenda na mabadiliko ya kitekinolojia na jinsi soko linavyokwenda na kueleza kwamba kunatofautiana na kutaka kwenda kadiri ya soko linavyotaka na kutaka kila mwandishi wa habari awe kama kiraka

Naye Mkurugenzi wa Radio Fadhila, Edwin Mpokasye, amewashukuru, VIKES, kwa mafunzo hayo na kusema yamekuja wakati mwafaka kwani wamepata weledi wa kuwajengea kufanyia kazi kwa ufanisi zaidi.

Amesema mafunzo hayo kwa ajili ya kutumia Mitandao ya Kijamii imewapatia weledi katika tasnia ya habari na kuahidi kutumia fursa hiyo ambayo wameipata