Radio Fadhila

World radio day at radio fadhila with school children

14 Febuari 2022, 11:23 mu

Katika kuadhimisha Siku ya Redio Duniani๐ŸŒ, ambayo kilele chake ni tarehe 13 mwezi huu, Redio Fadhila FM 95.0, imetoa fursa kwa kundi ambalo huenda halikupata nafasi ya kutembelea kituo chetu na kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo Redio.
Tumewapa nafasi wanafunzi wa shule ya Msingi Sabasaba-Masasi, ambapo wamepata kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo uandaaji wa vipindi na urushaji wa matangazo.
Nyuso zao zilijaa tabasamu na kwa hakika wamejifunza na kufarijika sana. Pengine tumetengeneza ndoto mpya ya baadhi yao kutamani kuwa wanahabari.
Sambamba na dhamira kuu ya maadhimisho inayosisitiza uaminifu wa Redio, wanafunzi wameweka wazi namna wanavyoiamini na kuitengemea Redio, hasa katika kujifunza๐Ÿ“š, kupata taarifa๐Ÿ“ฐ na kuburudika๐Ÿคธโ€โ™‚๏ธ na wameomba kupatiwa redio katika shule yao kama nyenzo mojawapo ya kujifunzia.
Na @georgepogyy_tz
#WorldRadioDay