Radio Fadhila

Halmashauri ya Wilaya ya Masasi imekabidhi Hundi ya Mikopo ya shilingi Milioni miamoja

1 February 2022, 11:32 AM

Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mkoano Mtwara imekabidhi Hundi ya Mikopo ya shilingi Milioni miamoja na hamsini na tano kwa vikundi 33 vya wanawake ,vijana ,na watu wenye ulemavu vilivyopo halmashauri hiyo .

Makabidhiano hayo yamefanyika February 1, 2022, katika ukumbi wa Mikutano uliopo Mbuyuni ambapo ni Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Masasi.

Afisa Maendeeleo ya jamii Neema Josephu ameeleza kuwa lengo la kutoa Mikopo hiyo ya asilimia kumi inayotokana na Mapato ya ndani ya Halmashauri ni kutaka kuwainua wanawake ,vijana na watu wenye ulemavu Kama utekelezaji wa Ilani ya chama Cha Mapinduzi .

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Masasi Bi Claudia Kitta amewaomba wanakikundi wote ambao wamepewa Mikopo hiyo kwenda kuzifanyia kazi Kama malengo yao waliyojiwekea wakati Wanaomba Mikopo hiyo Ili waweze kurejesha kwa wakati Na wengine ambao hawajawahi kupata waweze kupewa Mikopo hiyo.

Sambamba na hayo Mkuu wa wilaya ya Masasi Bi Claudia Kitta amekabidhi pikipiki Mbili kwa maafisa ugani wa kata ya Chiungutwa na Mwena ambazo zimetolewa na Wiazara ya Mifugo na Kilimo kwa lengo la kuwawezesha maafisa ugani kufanya kazi Kwa urahisi katika maeneo Yao ya kazi.