Radio Fadhila

BARAZA la Madiwani la halmashauri ya mji Masasi limepitisha rasimu ya makisio ya bajeti ya mapato

26 January 2022, 4:49 AM

BARAZA la Madiwani la halmashauri ya mji Masasi mkoani Mtwara limepitisha rasimu ya makisio ya bajeti ya mapato na matumizi ya halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha, 2022/2023 ya Sh.23.8 bilioni.

Madiwani hao wamepitisha bajeti hiyo ya mapato na matumizi kwa mwaka huo wa fedha hii leo katika kikao cha baraza la Madiwani cha kupokea, kujadili na kupitisha rasimu ya bajeti.Akiwasilisha rasimu hiyo ya mpango wa bajeti mbele ya Madiwani wa halmashauri hiyo kwa niaba ya mkurugenziwa halmashauri hiyo Eliasi Ntiruhungwa,afisa mipango wa halmashauri ya mji Masasi, Abirahi Mfinanga amesema kuwa katika mwaka wa fedha, 2022/2023 halmashauri ya mji Masasi imepanga kukusanya na kutumia kiasi cha fedha Sh.23.8 bilioni katika bajeti yake.

Ameeleza kuwa kati ya fedha hizo fedha zitokanazo na mapato ya ndani ya halmashauri ni Sh.2.6 bilioni na fedha za ruzuku toka serikali kuu ni zaidi ya Shilingi bilioni sita.Aidha,amesemua kuwa kiasi cha Sh 715 milioni zimetengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwa mwaka huo wa fedha.Kwa upande wake, mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Hashimu Namtumba amesema kuwa ili kuweza kufikia malengo ya bajeti hiyo inapaswa kuwepo na usimamizi mzuri wa ukusanyaji wa mapoto.

Naye mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Ntiruhungwa amesema kuwa ofisi yake pamoja na watendaji wa halmashauri watashirkiana vema na Madiwani katika kuhakikisha bajeti ya mwaka wa fedha, 2022/2023 inafikia malengo kama yalivyokusudiwa na kupendekezwa na Madiwani.Amesema halmashauri imeridhia kwa asilimia 100 kuyafanyia kazi mapendekezo yote yaliyotolewa na Madiwani hao juu ya bajeti hiyo ili kwa pamoja kuweza kuleta mandeleo ya wanamasasi.