Radio Fadhila

WANAWAKE WAJANE WAIOMBA SERIKALI KUWAWEZESHA KUJIKWAMUA KIUCHUMI

17 Disemba 2021, 3:58 mu

Umoja wa Wanawake Wajane Nchini (CCWWT) chini ya Mwenyekiti wake Bi. Rabia Ally Moyo umeiomba Serikali ya awamu ya sita chini ya Mama Samia Suluhu Hassan kuwawezesha kiuchumi kwa kuwapatia mikopo itakayowawezesha kufanya shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

Hayo yamesemwa katika kongamano la siku moja lililowakutanisha wajane zaidi ya 400 kutoka katika mikoa mbalimbali hapa Nchini ikiwemo Dares salaam, Ruvuma na Mtwara; lililofanyika Nanyumbu Mkoani Mtwara.

Kongamano hilo ambalo lilibeba hadhi ya kitaifa limefanyika Wilayani humo pamoja na mambo mengine limekusudia kuwajengea uwezo Wanawake kujitambua na kujiamini katika kutete haki zao ndani ya jamii, ambapo walitoa fursa kwa wadau wanaojishughulisha na masuala ya sheria na utetezi wa haki za binadamu Wilayani humo (H.P.O), kuwafundisha mada mbalimbali zinazopinga kuwafanyia ukatili wa kijinsia Wanawake na Watoto.