Radio Fadhila

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

17 Disemba 2021, 3:50 mu

                                 

ikumbukwe tu tarehe 13/12/2021 katika Mahakama ya Wilaya ya Masasi, ilitolewa hukumu ya kesi namba ECC.10/2021  iliyokuwa ikiwakabili washitakiwa RASHID MTIMA na mwenzake.

Washtakwa hao wanakabiliwa na makosa 02 kifungu cha 22 na 28 cha sheria ya TAKUKURU namba 11 ya mwaka 2007 ambapo wamekisababishia Chama cha Msingi Mkululu hasara ya Tshs 3,000,000/=.

Shauri hili lilikuwa likiendeshwa na mwanasheria wa TAKUKURU Wilaya ya masasi  CHARLES MTUNGILA.

Akisoma hukumu hiyo Mh. Kashusha ambaye ni ndiye aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo alieleza kuwa mshitakiwa namba moja na namba mbili wameonekana kuwa na hatia katika kesi hiyo.

Washtakiwa wote kila mmoja alihukumiwa kulipa faini ya Tsh 300,000/= au kwenda jela miaka 7