Radio Fadhila

Shule ya Sekondari Chanika Nguo yajengewa vyumba vinne

8 Disemba 2021, 3:17 mu

Shule ya Sekondari Chanika Nguo yajengewa vyumba vinne vya Madarasa vyenye thamani ya Shilingi Milioni 80.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marko Gaguti wakati akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Chanika Nguo pamoja na wananchi alipokuwa ziarani Wilayani Masasi kukagua miradi ya maendeleo ya Elimu.

Aidha Mkuu wa Mkoa ameagiza ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa ukamilike kabla ya tarehe 5 ya mwezi Disemba Mwaka huu 2021.