Radio Fadhila

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Dkt Festo Dugange amekuwa ziarani Wilayani Masasi

8 Disemba 2021, 3:26 mu

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Dkt Festo Dugange amekuwa ziarani Wilayani Masasi na kutembelea Halmashauri ya Mji Masasi ambapo amekagua ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya sekondari ya wasichana Masasi Shule ya sekondari Anna Abdallah na ujenzi wa kituo cha Afya Marambo

Kabla ya hapo alipokea taarifa ya maendeleo ya ujenzi huo kutoka Halmashauri ya Masasi Mji na Halmashauri ya Wilaya ya Masasi katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Masasi. Ameipongeza Halmashauri ya Masasi mji kwa kutumia vyema fedha zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya ujenzi huo kiasi cha Tsh Mill 820.