Radio Fadhila

Masasi-Kamati ya Lishe kuweka wazi bajeti yao.

8 Disemba 2021, 3:21 mu

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Masasi Mji Eliasi Ntirihungwa ameitaka Kamati ya Lishe kuweka wazi bajeti yao, Kwani serikali inataka kujua wadau wa taasisi mbali mbali nao wamechangia kiasi gani cha fedha na kupata makadirio ya bajeti ya mwaka mzima ili kuleta maendeleo.

Ameyasema hayo kwenye kikao cha kuandaa makadirio ya bajeti ya lishe ambapo amesema kamati ya lishe isizubae katika kuandaa bajeti kwani itawasaidia serikali kupata mjumuisho wa bajeti kwa mwaka mzima 2021.