Radio Fadhila

WAKULIMA wa zao la ufuta wa chama kikuu cha ushirika wa wakulima Masasi wamelipwa fedha zao

9 Julai 2021, 7:31 mu

WAKULIMA wa zao la ufuta wa chama kikuu cha ushirika wa wakulima Masasi-Mtwara (MAMCU) mkoani Mtwara wamelipwa fedha zao jumla ya sh.11,702,529,251 ambazo ni mauzo ya jumla ya kilo 5,002,275 katika minada miwili ya zao hilo iliyofanyika mwezi huu wa msimu wa 2021/2022

Hayo yamesemwa na Meneja wa Mamcu tawi la Masasi,Joseph Mmole alipokuwa akizungumza ofisini kwake juu ya mwenendo wa mauzo ya zao la ufuta kwa mnada wa kwanza na wapili.

Mmole amesema jumla ya minada miwili tayari imeshafanyika tangu kufunguliwa kwa msimu wa zao hilo mnamo juni mwaka huu ambapo mnada wa kwanza ulifanyika wilayani Nanyumbu juni 11

Amesema katika mnada huo wa kwanza jumla ya kilo za ufuta zipatazo 2,035,028 zenye thamani ya sh.4,598,809 ziliuzwa ambapo bei ya juu ilikuwa ni sh.2,262 na bei ya chini iliuzwa kwa sh.2,258

Mmole alieleza kuwa mnada wa pili umefanyika juni 18 katika kata ya Chiwale na kwenye mnada huo wakulima walikubali kuuza jumla ya kilo 2,967,247,247 kwa bei ya juu ya sh.2,452 huku bei ya chini ukiuzwa kwa sh.2,383 na jumla ya fedha za mauzo yam nada huo wa pili ni sh.7,103,855,442

Amesema jumla ya kilo za ufuta zilizouzwa katika minada yote miwili iliyofanyika hadi sasa ni 5,002,275, wenye jumla ya thamani ya sh.11,702,529,251

Mmole amesema tayari wakulima hao wameshalipwa fedha zao kupitia akaunti zao za benki ambapo fedha hungizwa kwenye vyama vyao vya msingi na vyama kwa shirikiana na mabenki fedha hizo za wakulima huingizwa katika akaunti zao za benki.

Aidha, baadhi ya wakulima waliozungumza na ukurasa huu wameopingeza serikali kwa kusimamizi mzuri wa mazao ya wakulima na kumpongeza rais Samia Suluhu kwa kuendelea kuwajali wakulima.