Radio Fadhila

TATEDO Kushirikiana na WWF yatoa majiko 2 na Sufuria 2 kupunguza uharibifu wa mazingira

20 Mei 2021, 11:35 mu

Shirika lisilo la kiserikali TATEDO linalo jihusisha na uendelezaji wa teknolojia na huduma za nishati endelevu tanzania, katika ukanda huu wa ruvuma linatekeleza Mladi wa kuleta mabadiliko katika sekta ya nishati na mradi huu unafaziliwa na WWF tanzania na kushirikiana hirika la maendeleo la swideni (SIDA). ikiwa ni rengo la kupunguza uharibifu wa matumizi makubwa ya nishati limetoa msaada wa majiko mawili na sufuria 2 zenye samani ya sh milioni tatu na laki mbili katika chuo cha maendeleo masasi (FDC)

Majiko hayo yanauwezo wa kupunguza matumizi ya kuni kwa zaidi ya 66% majiko hayo yametengenezwa mfumo mzuri wa kutoa moshi kupitia dohani kwa inje SHIMASAGO anayefanya kazi TATEDO anabainisha.

 

SHIMASAGO amesema katika mkoa wa mtwara wameshatoa majiko hayo katika vyuo viwili, ambapo ni chuo cha maendeleo wananchi mtawanya pamoja na chuo cha wananchi masasi.

Ametowa wito kwa jamii nzima kubadilika kujua teknolojia hizo zipo kama jamii inajenga shule basi ifikilie wanafunzi watakula hivyo nishati itahitajika kwani majiko hayo yanauwezo wa kukaa miaka 3 hadi 4 bila kufanyiwa lipea.

MKUU WA CHUO CHA MAENDELEO MASASI Akisoma taarifa ya matumizi ya nishati alisema chuo kinajumla ya wanafunzi 458 , hivyo kuwasababishia matumizi makubwa ya kuni katika mapishi kwa siku moja mita za ujazo 8 za kuni sawa na mizigo 32 za kuni hutumika.

CHUO CHA MAENDELEO MASASI kimetoa shukrani kwa WWF na TATEDO kwa kuwapa kipao mbele halimashauri ya mji masasi na halimashauri ya wilaya masasi kuwa sehemu ya wahamasishaji wa matumizi ya majiko sanifu ya kuni ya taasisi.

Akimwakilisha mkurugenzi mtendaji wa halimashauri ya wilaya ya masasi, Bi KULWA , alisema uzinduzi huo unaenda kuwa chachu ya uhifadhi wa mazingira na pia aliwaomba WWF kupitia taasisi ya TATEDO wasiishie hapo waendelee kufadhili tasisi zingine ambazo bado zinamatumizi ya kuni .

DANIEL NVELA ni mratibu wa mpango wa kuleta mabadiliko kutoka shirika la WWF ofisi ya masasi anaratibu program ya miaka 5 ili kushiriki kikamilifu katika kuhifadhi mazingira pamoja na mali asili na wananchi kunufaika

KULWA MAIGA ni afisa mazingira ya wilaya ya masasi alibainisha kuwa taasisi ya TATEDO wanaifahamu toka mwaka 2018 ,mwakajana walitambulusha mradi wa hifazi wa mazingira kwa njia ya majiko sanifu kwa ajili ya wananchi walioko vijijini ili kusaidia kupunguza matumizi ya kuni na amewaomba TATEDO iendeleE kutoa kwa taasisi zingine kwani baadhi ya taasisi ni chanzo za uharibifu wa mazingira