Radio Fadhila

Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi-CCM Wilaya ya Masasi wamlilia Rais Dkt. John Pombe Magufuli

23 Machi 2021, 9:12 mu

Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi-CCM Wilaya ya Masasi wamlilia Rais Dkt. John Pombe Magufuli na kueleza kuwa taifa limepoteza kiongozi shujaa na mpenda maendeleo na kwamba alikuwa ni mtetezi wa wananchi wanyonge hivyo wataendelea kumkumbuka milele. Wanachama hao leo Mach, 22 walifanya siku maalumu ya kukutana pamoja katika viwanja vya ofisi ya CCM ya wilaya Masasi kumuaga Dkt. Magufuli kwa kusaini kitabu cha maombelezo na kutoa salamu zao za maombolezo ya kumkumbuka na kuahidi kuyahenzi mambo yote mazuri ambayo ameyaacha.

CHAMA Cha Mapinduzi( CCM) Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara kimesema kuwa kitamkumbuka Hayati, Rais Dkt.John Pombe Magufuli kwa ufanikishaji wa miradi mikubwa ya kimaendeleo iliyofanyika Wilayani Masasi kwa kipindi cha uongozi wake wakati wa uhai wake. Baadhi ya miradi ambayo Rais Dkt. Magufuli ameifanikisha Wilayani Masasi ni ujenzi wa vituo vya afya, Zahanati, Madarasa, Miradi ya Maji, shule mpya za msingi ikiwemo shule ya kisasa Kitunda, miundombinu ya barabara , umeme vijijini Nk.hivyo CCM Masasi itamkumbuka daima. Hayo yamesemwa leo Mach, 22 na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, CCM ya Wilaya ya Masasi- Edward Mmavele kwa niaba ya wanachama, wakereketwa wa Chama hicho pamoja na wananchi wa Masasi kwa ujumla , alipokuwa akitoa salamu za maombolezo kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Masasi mbele ya wanachama wa CCM Masasi kwenye ofisi za Chama hicho hapa Masasi. Aidha, wanachama hao wa CCM wilaya ya Masasi walipata fursa ya kusaini kitabu Cha maombolezo kilichopo katika ofisi za Chama hicho ikiwa ni sehemu ya kushiriki kumuaga Rais Dkt. Magufuli ambapo kitaifa leo shughuli hiyo inafanyika jijini Dodoma. Mmavele amesema CCM wilaya ya Masasi kimesitishwa sana na kifo Cha Rais Dkt. Magufuli na kwamba Chama hicho kitamkumbuka kwa miradi ya maendeleo iliyotekelezwa Masasi ambayo imetumia mabilioni ya fedha kwa lengo la kuifanya Masasi kukua kiuchumi. Amesema kuwa kwa mambo yote mazuri aliyoyafanya Rais Dkt. Magufuli kwa wanamasasi na Chama kwa ujumla ikiwemo ujenzi wa ofisi za Chama ambapo Dkt. Magufuli alichangia kiasi cha fedha zaidi ya Sh.20 milioni ili kufanikisha ujenzi huo wa jengo la ofisi za Chama Cha Mapinduzi- CCM wilaya ya Masasi. Mmavele amesema CCM Wilaya ya Masasi kamwe hakitomsahau Rais Dkt. Magufuli kwa kuifanya nchi kuwa na maendeleo makubwa hivi sasa na kwamba Chama kitaendelea kumuhenzi na kuyaendeleza yale mazuri aliyokayapanga kuyatekeleza lakini ameyaacha na kutangulia mbele za haki. BURIANI DKT. JOHN POMBE MAGUFULI.CCM WILAYA MASASI.