Radio Fadhila

MKUU Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara., Selemani Mzee asaini kitabu cha maombolezo

23 Machi 2021, 9:22 mu

MKUU Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara., Selemani Mzee akisaini kitabu cha Kumbumbuku ya maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Rais Dkt. John Magufuli kilichotokea Machi, 17 mwaka huu, kitabu hicho cha maombelezo hayo kimefunguliwa kkatika ofisi ya mkuu ya wilaya ya Masasi. Aidha, Mkuu huyo wa wilaya, Selemani Mzee anawakaribisha wananchi wote wa Masasi kufika katika ofisi hizo kushiriki kusaini kitabu hiko kuungana na taifa kwa ujumla katika maombelezo haya. Kitabu hicho kitakuwepo katika ofisi hizo kuanzia majira ya saa 12 ; 00 asubuhi hadi saa 10 :00 jioni kila siku katika kipindi cha maombelezo..PUMZIKA kwa Amani , Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli , Tulikupenda sana lakini Mungu amekupenda zaidi.