Radio Fadhila

TANZIA: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Afariki Dunia

18 Machi 2021, 4:03 mu

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kifo cha Rais  wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kilichotokea Machi 17, 2021 katika hospitali ya Mzena Jijini  Dar es Salaam alipokuwa  akipatiwa matibabu ya  maradhi ya moyo.
 Rais  Magufuli alifikishwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Machi 6 mwaka huu na kuruhusiwa Machi 7, akaendelea na majukumu yake.

Hata hivyo, alipelekwa katika Hospitali ya Mzena Machi 14 baada ya kueleza kujisikia vibaya, ambapo amekuwa akipatiwa matbabu hadi umauti ulipomkuta.

Kufuatia msiba huo, Makamu wa Rais ametangaza siku 14 za maombolezo ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti.