Radio Fadhila

Ndoa Na Taraka Katika Jamii!!!

10 Machi 2021, 11:45 mu

Hakimu mkazi mfawidhi mahakama ya mwanzo lisekese masasi  LIGHTINESS  MASIMBA alipokuwa akizungumza na kipini cha amka na radio fadhila akizungumzia maswala ya ndoa na taraka ameeleza maana ya ndoa kwa mujibu wa sheria ya ndoa sheria number 29 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2019 inaeleza ndoa ni muunganiko wa hiaali baina ya mwanamke na mwanaume namuunganiko huo unakuwa na kusudi la kudumu katika maisha hayo yote pia amezungumzia  sheria inayo ruhusu mtoto kuolewa  akiwa chini ya umri wa mika 14 kwa izini ya wazazi au kuoa  akiwa nchini ya umri wa miaka 17 kwa izini yz wazazi

Kwa mujibu wa sheria  ya Tanzania hairuhusu ndoa ya jinsi moja (mwanamke kwa mwanamke au mwanaume kwa mwanaume)ili ndoa iwe halalila lazima ndoa inayofungwa mmoja awe mwanamke na mwingine awe mwanaume ndoa za Tanzania hairuhusu kuoana ndugu kwa ndugu  katika muunganiko wa ndoa kuna habari za taraka na kuna migogoro ya ndoa

KIDA MWANGESI wakili wa kujitegemea  kutoka SPERO ATTORNEYS  masasi amezungumzia ndoa badilifu ni  ndoa inayokuwa na mazaifu kama mmoja akawa na magonjwa ya kuridhi ,changamoto ya masawala ya uzazi , changamoto katika maswala ya kushiriki tendo la ndoa,   kutengana zaidi ya miaka mitatu ,kifungo kisipo pungua miaka mitano, mweza kupata kichaa  hivyo mahakama inaweza kutengua ndoa kwa mujibu wa sheria

Pia amezungumzia maswala ya taraka kunabaadhi ya vitu ambavyo hufikiwa mpaka mtu anaamua kutoa taraka kama vile ukatili ambao umevuka kiwango kuhatarisha  maisha na ametoa hamasa kuwa unapo ona ukatili umezidi sana katika ndoa chukua hatua  ya kuomba taraka au kutoa taarifa polisi  ili kunusuru hasara inayoweza kutokea mwandoa mmoja anayeta kuimba mahakama itengue ndoa mahakamani akiwa ambatanisha pamoja na fomu no3 ambayo ameipata kutoka baraza la upatanishi

Huu ni mwendelezo wa mazungumza na wanasheria amabao hufikaradio fadhila katika kipindi cha amka na radio fadhila  kwa ajili ya kuendesha maada mbalimbali zinazo husu sheria ikiwemo migogoro ya aridhi .