Radio Fadhila

Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoa wa mtwara yafanyika wilayani masasi!

8 Machi 2021, 4:01 um

Maadhimisho ya siku ya wanawake dunia ambayo huazimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 8 mwezi wa 3 yamefikiwa kilele chake hii leo , maadhimisho hayo. katika mkoa wa mtwara yamiadhishwa katika wilaya ya msasasi uwanja wa boma na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali  wa mkoa na wilaya , mkuu wa wilaya ya msasi mh. seleman mzee na mgeni rasmi katika sherehe hizo alikuwa ni mkuu wa mkoa wa mtwara mh  MH GELASIUS BYAKANWA  ya kiwa yamebeba kauli mbiu  isemayo  MWANAMKE KATIKA UONGOZI  CHACHU YA KUFIKIA DUNIA YENYE USAWA

Maadhimisho hayo yalienda sambamba na maandamano ya kinamama yakiwa na mabango yaliyobeba jumbe tofauti tofauti kuelekea uwanja wa boma , baadhi ya wajasilia mali wanawake na vikundi mbalimbali  walileta bidhaa zao na kuziuzi katika maadhimisho hayo .

Mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa mtwara mh gelasius byakanwa aliwapongeza wanawake kwa kazi mbalimbali walizo zifanya katika kipindi chote cha week katika kuelekea maadhimisho haya ya siku ya mwanamke duniani

Pia mkuu wa mkoa wa alisema wanawake wanayo nafasi ya kushiriki katika ukombozi wa  jamii hii kama vile alivyopatikana makamo wa rais wa  jamhuri ya muungano wa Tanzania samia suruhu, naibu spika wa bunge, waziri wa afya ,pia wa kuu wa mikoa wanawake pamoja na wakuu wa wilaya  kama mkuu wa wilaya ya newala

Ikumbukwe tu maadhimisho haya ya Siku ya Wanawake Duniani huadhimishwa tarehe 8 Machi ya kila mwaka. Siku hiyo ilianza kuadhimishwa tarehe 8 Machi 1975 baada ya Umoja wa Mataifa kuridhia siku hii kutumika  kama siku rasmi ya kuikumbusha dunia juu ya haki za wanawake.