Radio Fadhila

Simba itakaribishwa na African Lyon

26 Febuari 2021, 6:05 mu

IKIWA Uwanja wa Mkapa leo Simba itakaribishwa na African Lyon kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho ambao utachezwa majira ya saa 1:00 usiku.

Chini ya Kocha Mkuu, Didier Gomes unakuwa ni mchezo wake wa kwanza kwenye Kombe la Shirikisho baada ya kurithi mikoba ya Sven Vandenbroeck ambaye alitwaa taji hilo msimu uliopita. 

Hiki hapa ni kikosi cha Simba kinachotarajiwa kuanza leo dhidi ya African Lyon:-

Beno Kakolanya

Duchu

Gadiel Michael

Kenedy Juma

Ibrahim Ame

Jonas Mkude

Said Ndemla 

Meddie Kagere

Bernard Morrison

Miraji Athuman

Ibrahim Ajibu