Radio Fadhila

BARAZA la Madiwani lapitisha Rasimu ya Bajeti 2021/2022

26 Febuari 2021, 5:14 mu

BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Masasi mkoani Mtwara limepitisha Rasimu ya Mpango wa Bajeti kwa Mwaka wa fedha 2021/2022,Mpango huo umepitishwa katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika jana tarehe 24, Febuari katika ukumbi wa Halmashauri hiyo Mbuyuni Baraza hilo limepitisha Rasimu ya Bajeti yenye makisio yenye thamani ya Sh.44,397,290,000,00 (Bilioni) .Katika bajeti hiyo ,Mishahara imepanga kutumia Sh.27,696,792,000,00.Miradi ya Maendeleo Sh. 11,898,954,000,00. Mapato ya ndani ya Halmashauri Sh.3,538,673,000,00. Matumizi mengineyo ni Sh.1.262,871,000,00 Na kufanya Rasimu hiyo ya Mpango wa bajeti kuwa jumla kuu Sh.bilioni , 44,397,290,000,00 Ka upande mwingine Madiwani hao wamepongeza uandaaji wa Bajeti hiyo ya mwaka huu wa 2021/2022 na kukiri kwamba ina mabadiliko makubwa ukilinganisha na Bajeti ya mwaka wa fedha uliopita wa 2020/2021 ambayo ilikuwa ni Sh.34,639,132,000,00 Aidha,Madiwani hao wameshauri pia Halmashauri hiyo kuendelea kuongeza kubuni vyanzo vipya vya Mapato ikiwemo kujenga stendi mpya ya magari katika eneo la Mbuyuni, ujenzi wa Maghala na vyanzo vingine amvayo kwa pamoja vitasaidia Halmashauri kuweza kupata Mapato kwa wingi hatimaye kuweza kutekeleza vema Bajeti zinazopangwa na Halmashauri hiyo. Akifunga kikao hicho, Makamu mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Athony Chihako ambaye ndiye aliyeendesha kikao kwa niaba ya mwenyekiti,Chiahako ambaye pia ni Diwani wa kata ya Msikisi, amesema kuwa bajeti hiyo ili iweze kutekelezwa kama ilivyopangwa inategemea ukusanyaji bora wa mapato kwa Halmashauri.