Radio Fadhila

NAHODHA wa Al Ahly, Aiman Ashraf atowa angalizo

23 Febuari 2021, 4:49 mu

NAHODHA wa Al Ahly, Aiman Ashraf amesema kuwa wamekuja Dar kwa ajili ya kupata ushindi mbele ya wapinzani wao Simba.
Kesho, Februari 23 Al Ahly itakaribishwa na Simba, saa 10:00 kucheza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ni hatua ya makundi.
Mchezo huo unatarajiwa kuchukua jumla ya mashabiki 30,000 kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Afrika,(Caf) kwa ajili ya kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.
Nahodha huyo amesema:”Lengo letu kubwa ni kutwaa ubingwa na tunajua tunacheza na timu kubwa hivyo hatutadharau jambo lolote.
“Kuhusu muda wa mechi hauwezi kuwa kikwazo kwetu. Tumekuja kupambana tupo tayari kwa ajili ya mchezo huo hivyo tutaingia kwa tahadhari na tunawaheshimu wapinzani,”.