Radio Fadhila

Mwamuzi Lucien Toudignon wa Benin Ashambuliwa na wachezaji

23 Febuari 2021, 4:46 mu

Mwamuzi Lucien Toudignon wa Benin jana akiwa amelazwa kwenye hospital nchini Burkina Faso baada ya kushambuliwa na wachezaji wa klabu ya Bouenguidi ya Gambia kwenye mchezo wa mkondo wa pili wa kufuzu makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika (Caf Confederation Cup) dhidi ya Salitas FC ya Burkina Faso. Bouenguidi ilifungwa kwa magoli 3-1 na kutolewa kwa jumla ya magoli 3-2.