Radio Fadhila

PRINCE Dube,Azam FC, ATUPIA TENA

19 Febuari 2021, 10:17 mu

PRINCE Dube, mshambuliaji namba moja ndani ya kikosi cha Azam FC, usiku wa kuamkia leo amepachika bao lake la 7 ndani ya ardhi ya Bongo akiwa ni kinara wa utupiaji ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na George Lwandamina. 

Alifunga bao lake hili Uwanja wa Azam FC wakati wakishinda mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City na kufanya wasepe jumla na pointi sita za timu hiyo inayopambana kujinasua kutoka Kwenye hatari ya kushuka Daraja.

Bao la mapema kwa Azam FC lilifungwa na Idd Seleman, ‘Nado’ dakika ya 5 na Dube alipachika bao hilo dakika ya 30 huku la kufuta machozi kwa Mbeya City likifungwa na David Mwasa dakika ya 69.

Mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Sokoine,  Azam FC ilishinda bao 1-0 na jana ilishinda mabao 2-1 hivyo wamesepa na pointi sita jumla mbele ya Mbeya City.

Ni muda mfupi ameanza kurejesha ushkaji wake na nyavu baada ya kubadili muonekano kwa kuwa sasa ana upara kichwani.

Azam FC kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ipo nafasi ya tatu ikiwa imecheza jumla ya 20 na ina pointi 33.

Mbeya City ipo nafasi ya 17 imecheza jumla ya 20 ina pointi 15 kinara wa ligi ni Yanga akiwa na pointi 46 imecheza mechi 20.