Radio Fadhila

Barcelona wanyooshwa na PSG mabao 4-1

17 Febuari 2021, 9:56 mu

LICHA ya kutupia bao la kwanza mapema dakika ya 27 kwa mkwaju wa penalti,kupitia kwa Lionel Messi bado ilikubali kichapo cha mabao 4-1 mbele ya PSG, mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, hatua ya 16 bora.

Barcelona imekuwa kwenye wakati mgumu kupata matokeo ndani ya uwanja huku tatizo likitajwa kuwa kwenye ukuta wao ambao haupo imara.

Nyota wa mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa alikuwa ni Kylian Mbappe wa PSG ambaye alisepa na mpira wake baada ya kutupia hat trick.

Alianza kutupia dakika ya 32,65 na 85 na msumari mmoja kwa PSG ulipachikwa na Moise Kean.

Barcelona wakiwa uwanja wao wa nyumbani, Camp Nou wao walipiga jumla ya mashuti 12 na manne yalilenga lango huku PSG wakipiga jumla ya mashuti 16 na 9 yalilenga lango.

Ina kazi ya kupindua meza kibabe kwenye mchezo wa marudio ambapo watakuwa ugenini jambo ambalo litawapa nafasi ya kusonga mbele ikiwa watapoteza safari yao itakuwa imewadia.