Radio Fadhila

Msanii wa Bongofleva Ilunga Khalifa maarufu C Pwaa amefariki Dunia

17 Januari 2021, 11:57 mu

Msanii wa Bongofleva Ilunga Khalifa maarufu C Pwaa amefariki Dunia Alfajiri ya kuamkia leo akiwa anapatiwa matibabu Hospitali ya Taifa Muhimbili., Ndugu wa karibu wa C Pwaa amethibitisha kuwa Pwaa alikuwa anaugua Pneumonia na alifikishwa Hospitali kwa matibabu, hali yake haikuwa njema hadi umauti unamkuta.Enzi za uhai wake C Pwaa alifanya vizuri akiwa na kundi la Park Lane pamoja na Suma Lee ambapo walitoa ngoma kama Nafasi Nyingine na Aisha, na baadaye alitoa ngoma zake nje ya kundi zikiwemo Action, Problem, So Pwaa, Six in the Morning nk