Radio Fadhila

Kaya Zaidi Ya 40 Katika Vijiji Vya Kivukoni Na Chiwale Zakosa Makazi

31 December 2020, 3:29 AM

Kaya zaidi ya 40 katika vijiji vya Kivukoni na Chiwale vilivyopo kata ya Chiwale Halmashauri ya wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara zakosa makazi baada ya mvua iliyoambatana na upepo mkali kuezua paa na kubomoa Nyumba zipatazo 42 katika vijiji hivyo.
Mvua hiyo iliyonyesha siku ya Disemba 25 ambapo ilipelekea nyumba hizo kubomoka kwa kiasi hicho.
Aidha,Wananchi hao wameiomba serikali kuwapatia msaada ikiwemo vifaa kama vile bati, mbao na misumari ili waweze kujenga upya nyumba zao hatimaye waweze kurejea kuishi na familia zao ambapo kwa sasa wanalazimika katika nyumba za ndugu na jamaa zao kwa muda.
Kamati ya maafa ikioongozwa na mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Masasi, Changwa Mkwazu imeshafika katika vijiji hivyo kwa lengo la kujionea hali halisi ya tukio hilo sambamba na kuwapa pole waarithika wa mahafa hayo.
Aidha, wananchi wameshauriwa kuchukua tahadhari katika kipindi cha mvua ikiwemo kuzingatia kanuni bora za ujenzi wa majengo ili kuepeka matukio kama hayo ya kubomoka majengo yao.

Chanzo-Hamisi Abdelehemani Nasiri