Radio Fadhila

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya mji Masasi, Gimbana Ntavyo awataka wasimamizi wa uchaguzi kufanya kazi kulingana na kiapo

26 Oktoba 2020, 4:03 mu

MSIMAMIZI wa Uchaguzi jimbo la Masasi mjini, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya mji Masasi, Gimbana Ntavyo( pichani katikati) amewataka Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi wa vituo vya kupigia kura jimbo hilo la Masasi mjini kwenda kufanya kazi zao kwa kuzingatia kiapo walichoapa Ntavyoaliyasema hayo hii leo oktoba 25 wakati alipokuwa akiwaapisha wasimamizi hao wasaidizi wa uchaguzi wa jimbo la Masasi mjini zaidi ya 600 ikiwa ni maandalizi ya kuelekea uchaguzi mkuu oktoba 28 Alisema wasimamizi hao wanapaswa kutambua kuwa majukumu yao ni muhimu sana katika kufanikisha zoezi zima la uchaguzi huo kutokuwa na dosari hivyo uwajibikaji wao mzuri katika usimamizi wao utaleta ufanisi kufanya uchaguzi uwe wa haki. Ntavyo alisema kila msimamiz wa kituo cha upigaji kura ajiepushe kufungaamana na Chama chochote cha siasa na ahakikishe anatenda haki kwa wapiga kura jambo ambalo litaondoa adha na malalamiko kwenye vituo vya kupiga kura. Sambamba na kula kiapo pia wasimamizi hao wamepatiwa mafunzo maalumu ya utekelezaji wa majukumu yao ili ifikapo oktoba 28 mwaka huu ya siku kupiga kura waweze kutimiza majukumu hayo kikamilifu.