Radio Ahmadiyya

Zahanati Mnyawa mikononi mwa mkuu wa mkoa

3 February 2023, 12:14 pm

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Con. Ahmed Abbas akizungumza na wanainchi katika kijiji cha Mnyawa kilichopo halmashauri ya wilaya ya Tandahimba.

Wameiomba serikali kusaidia ukamilishaji wa ujenzi wa kituo cha afya ili kuwapunguzia adha ya kujifungulia majumbani mwao.

Na Hamza Ally

Mkuu wa mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas amemwagiza Mhandisi wa wilaya ya Tandahimba m kufanya tathmini ya gharama za kumaliza ujenzi kwenye jengo la hospitali ya Kijiji cha Mnyau ambacho kimesimama kwa muda mrefu, ili awashawishi wadau mbalimbali wa maendeleo kuunga mkono jitihada za wananchi ambao wameanzisha ujenzi huo.

Kanali Abbas mesema hayo mara baada ya kufanya ziara ya kikazi ya siku moja wilayani Tandahimba na kutembelea eneo linakojengwa kituo hiko.

Aniletee kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa nami nitakapokuwa nazunguka kutafuta wadau wa maendeleo niwaombe wanisaidie kwa ajili ya kituo hiki.

Aniletee kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa nami nitakapokuwa nazunguka kutafuta wadau wa maendeleo niwaombe wanisaidie kwa ajili ya kituo hiki.Con. Ahmed Abbas.

Sauti ya Con. Ahmed Abbas.- Mkuu wa mkoa wa Mtwara

Nao baadhi ya Wakazi wa Kijiji cha Mnyawa kilichopo halmashauri ya wilaya ya Tandahimba Mkoani Mtwara, wameiomba serikali kusaidia ukamilishaji wa ujenzi wa kituo cha afya kijijini hapo, ili kuwapunguzia adha ya kujifungulia majumbani mwao.

Kwa mfano mama mjawazito anapata shida, japokuwa Hospitali ipo karibu sasa mtu mwingine akianza uchungu inakuwa shida kwasababu usafiri hakuna wakati mwingine wanajifungulia ndani tu kwa kukosa usafiri.

Wanakijiji Mnyawa