Pangani FM

Waandishi wa Habari waanza mafunzo ya mguso Dodoma.

18 March 2023, 4:39 pm

Baadhi ya Waandishi wa Habari washiriki wa mafunzo hayo wakijadili hoja zilizoibuka kwenye mafunzo. Picha na Erick Mallya

Na Erick Mallya

Waandishi wa Habari kutoka vituo 19 vya Tanzania bara na visiwani wameanza mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo katika Kuimarisha utangazaji wa jinsia ndani na kupitia vyombo vya Habari.

Mafunzo hayo yanayoendeshwa na Shirika la UZIKWASA lililopo wilayani Pangani Mkoani Tanga kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi na Utamaduni (UNESCO) yameanza Ijumaa Machi 17 na yanatarajiwa kumalizika machi 19 mwaka huu katika moja ya kumbi za mikutano za Royal village jijini Dodoma.

Sauti za waandishi wa Habari washriki wa mafunzo hayo.
Mwezeshaji kutoka Shirika la UZIKWASA Bw, Edward Saguti akendesha mjadala katika mafunzo hayo.

Kwa miaka mingi Shirika la UZIKWASA limekuwa likitoa mafunzo ya ‘mguso’ ambayo yamekuwa yakiwawezesha watu binafsi kutafakari nafasi zao katika kuchochea mabadiliko chanya pamoja na mabadiliko ya kitaasisi na Jamii kwa ujumla.

Mwandishi wa Habari Benedict Ngelangela kutoka Dodoma FM akichangia mjadala katika mafunzo hayo.

Wanufaika wa mafunzo hayo wamekuwa vongozi wa dini, viongozi wa taasisi, waandishi wa habari, vongozi wa kisiasa na wale wanaosimamia masuala ya Jinsia na Mazingira.

Faida za mafunzo hayo zimetambulika katika ngazi ya Kitaifa na Kimataifa.

Bi.Salvata Kalanga kutoka Shirika la UZIKWASA akiendesha sehemu ya mafunzo hayo. Picha na Erick Mallya

Mwezeshaji kutoka shirika la UZIKWASA Bi.Salvata kalanga amesema kuwa mategemeo kutokana na mafunzo hayo n kuwawezesha waandishi wa Habari kujimulika na kufanya tathmini binfafsi itakayochochea mabadiliko miongon mwao na vituo wanavyohudumu hasa katika masuala ya kiuongozi na Jinsia.

Sauti ya Mwezeshaji wa Shirika la UZIKWASA Bi. Salvata Kalanga